Hii hapa Bei ya Cement ya Dangote

Dangote Cement Mtwara kiwanda kinachosemekana kuwa kikubwa zaidi Afrika mashariki na Afrika yote kwa ujumla kwa mara ya kwanza kimeanza kusambaza saruji yake kuanzia Tarehe 21 February 2016
Kiwanda hicho ambacho ni tegemeo jipya kwa wakazi wa mikoa kusini kama Mtwara na Lindi awali kiliahidi ajira nyingi ya wakazi wa mikoa hiyo na watanzania kwa ujumla.. Hivyo ni wakati halisi sasa kwa watanzania kuchangamkia kazi na tenda zitakotolewa na kiwanda hicho katika kipindi hiki ambacho usambazaji wa saruji umeanza.
Saruji hiyo kwa sasa tayari ipo madukani na inapatikana kwa bei nafuu ya Tsh 13,500 tofauti na saruji kutoka viwanda vingine.

Post a Comment

0 Comments