Ulikuwa unafuatilia majaribio ya mtanzania Farid Hispania? C.E.O wa Azam FC ana taarifa hii

Baada ya kurejea kwa Farid Musa kutokea
Hispania alipokuwa anafanya majaribio
katika klabu ya Deportive Tenerife ya Ligi
daraja la kwanza Hispania (Segunda) , kila
mtanzania anatamani kujua nini kinaendelea
kwa staa huyo wa Azam FC na Taifa Stars.
Mwanzoni taarifa zilisikika kuwa kafaulu
majaribio lakini mazungumzo kati ya Azam
FC na Tenerife hayajafikiwa C.E.O wa Azam
FC Saad Kawemba katoa taarifa rasmi
“Ni kweli Farid amefuzu na kuna makubaliano
tunafikia kwa ajili ya maslahi ya mchezaji,
kwanza wanapaswa wampe muda sio akishindwa
kufanya vizuri mechi moja wamuache hapana
wanapaswa wampe muda”

Post a Comment

0 Comments