DIAMOND PLATNUMZ AKABIDHI MADAWATI 600 KWA MKUU WA MKOA WA DAR, PAUL MAKONDA

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva Naseeb Abdul maarufu Diamond Platnumz leo amekabidhi mchango wa madawati 600 kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam, Paul Makonda.
Diamond Platnumz ametoa mchango huo kufuatia kampeni inayoendelea nchi nzima ya kuchangia madawati ili kuwawezesha wanafunzi kuwa na mazingira mazuri ya kusomea kwa lengo la kuinua elimu nchini.
Diamond Platnumz amekabidhi madwati hayo kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda mapema leo asubuhi.

Post a Comment

0 Comments