TANZIA; gwiji wa miondoko ya taarabu kafariki dunia

Habari za kusikitisha zimetufikia muda huu kuwa malkia wa Tarabu nchini Bi. Shakila Saidi amefariki dunia jioni ya jana muda mfupi baada ya kuanguka na kukimbizwa hospitali ya karibu na nyumbani kwake Mbagala Charambe jijini Dar es salaam. Kwa mujibu wa familia ya marehemu, Bi Shakila hakuwa anaumwa ila alianguka ghafla na alipofikishwa hospitali akakata roho. Taarifa kamili tutawaletea mara tu tutapozipata.
MOLA AILAZE PEMA ROHO YA MAREHEMU - AMINA

Post a Comment

0 Comments