Makala kuhusu kisiwa kilichopo katika ziwa Nyasa kilichobeba historia ya kusisimua

KISIWA WALICHOKUWA WANAISHI WENYE UKOMA ZIWA NYASA
Kinachooneka kwa mbali katika picha ya kwanza ni kisiwa cha Puulu kilichopo ziwa Nyasa kata ya Liuli Wilaya ya Nyasa Mkoa wa Ruvuma, ambacho kina utalii wa kihistoria ambapo mwaka 1917 katika kisiwa hicho walikuwa wanaishi watu wenye ugonjwa wa ukoma ambao walitengwa na serikali ya ukoloni wa Kijerumani wakihofia watu hao kuwaambukiza wengine ukoma.Hata hivyo mara baada ya kupata Uhuru mwaka 1961 Serikali ya Awamu ya Kwanza chini ya Baba wa Taifa Mwl.Julius Nyerere iliamua kuwaondoa watu hao katika kisiwa hicho.Mwaka 1973 baada ya kuwajengea makazi mapya katika Kijiji cha Ngehe Kata ya Kihagara Wilaya ya Nyasa ambao wanaendelea kuishi hadi leo.Kituo hicho kipo chini ya Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto.




Post a Comment

0 Comments