MJUE FIDEL CASTRO ALIYEIFUNGIA VIOO MAREKANI KWA MIAKA 50


                                                           FIDEL CASTRO
                                                     

Ni baada ya miaka 50 kupita ya vita ya kutoelewana hatimaye Desemba 17, 2014 Marekani na Cuba zilifikia makubaliano. Ikulu ya Marekani (White House) ilitangaza kuwa Marekani imerejesha mahusiano ya kidiplomasia na taifa la Cuba ambalo ni kisiwa kilichopo Maili 90 tu kutoka pwani ya Florida, na kufungua ubalozi huko kwa mara ya kwanza tangu Dwight Eisenhower akiwa Rais.

                                    fidel_castro
 

Fidel Castro, kiongozi wa zamani wa Cuba aliyeongoza mapinduzi ya Kikomunisti na kuweka misimamo yake dhidi ya mataifa mengine, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 90. Ni miaka zaidi ya 50 tangu asitishe uhusiano wa Cuba na Marekani kabla ya kubariki tena uhusiano huo mwaka 2014.

Taarifa ya Rais Raul Castro ambaye ni mdogo wake na Fidel Imesema “Amiri jeshi mkuu wa mapinduzi ya Cuba alifariki dunia saa 22:29 usiku huu wa Jumamosi. Fidel Castro alitawala Cuba kama taifa la chama kimoja kwa karibu miaka 50 kabla ya kakake Raul kuchukua hatamu 2008.FIDEL CASTRO

Fidel Castro alizaliwa Agosti 13 mwaka 1926, mkoa wa Kaskazini Mashariki wa Oriente nchini Cuba katika familia iliyokuwa na umaarufu kwa kilimo cha miwa. Alijiunga na siasa za mapinduzi akiwa na umri mdogo sana.
Kama ilivyokuwa kwa Hayati Nelson Mandela wa Afrika Kusini kukaa jela ndivyo ilivyokuwa kwa Fidel Castro ambaye alitumikia miaka miwili jela kwa kuongoza mapinduzi. Alipotoka alienda mafichoni nchini Mexico. Mwaka 1956 alirudi na chama chake cha mapinduzi kikaongoza. Castro mwishowe akapata mamlaka ya kuiongoza Cuba tarehe 1, mwaka 1959, kama Waziri Mkuu kwa kumshinda Fulgencio Batista.
FIDEL CASTRO

Mwaka 1961,Castrol aliongoza kikosi chake cha jeshi dhidi ya raia wa Cuba 1,500 waliokuwa uhamishoni, wakifadhiliwa na CIA, walivamia Bay of Pigs ili kuipindua serikali yake. Alipata jaribio kubwa mwaka 1962, pale rais wa Marekani John Kennedy alipomuonya kuondoa makombora yake kutoka Cuba.
Mwishowe, viongozi Nikita Khrushchev na Castro waliondoa makombora na tishio la vita vya nyuklia vikazuiwa. Amri jeshi mkuu huyo alipenda kushiriki mchezo wa Baseball. Aliwahi kuonekana akicheza katika chuo cha ualimu huko Sierra Maestra mwaka wa 1962.
FFIDEL CASTRO

Wacuba wengi walimchukulia kama dikteta wa ukandamizaji. Mamia ya raia wa Cuba walikimbia makwao,kuelekea Marekani kwa kutumia maboti yaliyokuwa hatari. Lakini Fidel Castrol alipata uungwaji mkono kuwa miongoni mwa viongozi waliohudumu kwa miaka mingi duniani
Castro alianza kuugua miaka ya 2000, lakini aliendelea na madaraka hadi mwaka 2008 baada ya kufanyiwa upasuaji wa utumbo, alimkabidhi rasmi madaraka ya urais mdogo wake Raul. Alioneka mara chache kabla ya kung’atuka madarakani Februari 24 mwaka 2008.

Post a Comment

0 Comments