CIRO NI BALAA, ANAMNYIMA USINGIZI CR 7


CIRO Immobile anakipiga ndani ya Lazio inayoshiriki Serie A ni mbabe wa kucheka na nyavu.

Ametupia jumla ya mabao 25 ndani ya Ligi hiyo akimtupa kwa mabao matano Cristiano Ronaldo wa Juventus mwenye mabao 20.


Huyu ni mshambuliaji mweye miaka 29 anayemyima usingizi CR 7.

Nyota huyo pia sio mchoyo ametoa jumla ya asisti 6 zilizoleta mabao.

Amecheza dakika 1,922 ana wastani wa kutupia bao moja kila baada ya dakika 77.

Post a Comment

0 Comments