JB kustaafu kuigiza filamu, kazi atakayofanya ndio hii….

Bongo Movie legend na super staa JB Aka Jacob Stephen ametumia instagram yake kutupa habari muhimu kuhusu maisha yake ya kazi za filamu.
JB ametangaza rasmi kuwa muda wowote atapumzika kuigiza na ataanza kuwa mtayarishaji tu wa filamu.
Leo August 6 2016 JB aliandika ujumbe huu Instagram “ Nimekuwa nikipokea simu nyingi na sms toka kwa wapenzi wangu kwa nini napunguza kutoa movie…jamani naomba niwaambie ukweli..najiandaa kupumzika kuigiza…lakini najitengeneza kuwa producer mkubwa zaidi…ndio maana natengeneza hata Tamthilia…nimeigiza tangu 1998 hadi sasa..nakaribia 50years…kwa umri wangu natakiwa niwekeze zaidi kwa vijana ambao naamini wanaweza kufanya vizuri zaidi…baada ya kalambati lobo nitafanya movie yangu moja ya mwisho na kazi itakayo baki ni kuwasaidia vijana kupitia jerusalem…nawapenda sana na asanteni sana kwa kuniunga mkono…hamjawahi kuniangusha..nawapenda sana..jb..erickford..danija..dj ben..bonge la bwana..mzee wa swagga..Jacob stephene..


Post a Comment

0 Comments