Nahreel na Aika wa Navy Kenzo kujenga nyumba ya kifahari,itagharimu shilingi ngapi..

Msanii wa bongo fleva Nahreel ambaye pamoja na mpenzi wake wanaunda kundi la Navy Kenzo ameweka wazi kuwa yeye na mpenzi wake huyo wameanza kujenga nyumba ya kifahari itakayogharimu takribani shilingi milioni 700 za kibongo.
Akihojiwa kwenye kipindi cha Ujenzi cha East Africa Nahreel amesema nyumba hiyo wanayoijenga itakuwa ya kisasa zaidi na kutakuwa na bar humo humo ndani.
Tumechoka kukaa kwenye nyumba za kupanga tukaamua tutumie tulivyovipata kujenga nyumba yetu ambayo itagharimu milioni 700 ambapo itakuwa ni nyumba ya kisasa na itakuwa na bar ndani yake ” alisema Nahreel na kuwaasa wasanii wawekeze ikiwa bado muziki unalipa kwani biashara hiyo bado haieleweki kuna wakati inalipa na wakati mwingine hailipi.

Post a Comment

0 Comments