Hifadhi ya taifa ya Serengeti, yenye
ukubwa wa kilometa za mraba 14,763, ni
hifadhi ya pili kwa ukubwa nchini ( baada
ya Hifadhi ya Taifa ya Ruaha).
Serengeti ni moja kati ya hifadhi maarufu
sana duniani. Umaarufu wa hifadhi hii
unatokana na misafara mirefu ya nyumbu
wanao hama kwa makundi makubwa
kutoka upande mmoja wa mbuga hadi
mwingine, na kuvuka mpaka wa Tanzania
hadi hifadhi ya taifa ya maasai mara
nchini Kenya. Wakichagizwa na mvua kila
mwaka zaidi ya nyumbu milioni moja,
pundamilia 200,000, swala 300,000 huunga
misafara ya kutafuta malisho na maji.
Uhamaji huu umeipataia sifa ya kuwa
moja ya maajabu saba ya asili ya Afrika.
Hifadhi ya Serengeti pia ni maarufuu kwa
wanyama walao nyama kama chui na
simba. Ukubwa wa hifadhi hii umesaidia
sana kudumisha uhai wa wanyama walio
katika hatari ya kutoweka kama faru
weusi na duma. Uwapo Serengeti
utashuhudia wawindaji kama duma
wanavyowinda, aidha zipo aina
mbalimbali zaidi ya 500 za ndege.
Leo kwa ufupi, tutakupatia mambo kumi
(10) kuhusu Hifadhi ya Serengeti ambayo
ungependa kuyajua na kusimilua kwa
wenzanko ambao hawakupata kuyajua;
Mfumo wa Mazingira wa hifadhi ya taifa
Serengeti ni kongwe katika dunia. Hifadhi
hii inatunza viumbe hai mbalimbali
ikiwemo mimea na wanyama ambavyo
vingine havipatikani mahali popote
duniani.
2. Serengeti ni nyumba ya moja ya
maajabu ya asili saba ya dunia. Zaidi ya
nyumbu milioni moja uhama kwa kuvuka
mto Mara na kuelekea hifadhi ya taifa ya
Maasai Mara kwa upande wa Kenya katika
kutafuta malisho yao. Na hukaa Kenya
kwa mwezi mmoja tu na miezi iliyobaki
hutumia mda wao wakiwa Tanzania
3. Katika miaka zaidi ya milioni moja
iliyopita, hifadhi ya Serengeti imebaki
kuwa ya asili kwa kiasi kikubwa bila
kuathiriwa na mabadiliko ya kimazingira.
Wanyama pori, mimea na mikondo ya maji
bado kwa kiasi kikubwa ni ya asili kama
ilikuwa miaka milioni moja iliyopita. Kwa
kushangaza, mabaki ya zamani ya mtu
(miaka milioni 2 iliyopita) yaligunduliwa
hapa na mtu maarufu Afrika Mashariki
archaeologist, Dr. Leakey.
4. Watalii wengi huvutiwa na Hifadhi hii
na kushuhudia zaidi ya nyumbu milioni
moja wakiwa wanahama kwa kufatilia
malisho yao. Hata hivyo, punda milia pia
huhama pamoja na nyumbu, angalau kwa
idadi ndogo.
5. Maelfu ya wanyama wanaohama
wengine hushindwa kukamilisha safari yao
kutokana na kuliwa na mamba na
wanyama wengine walao nyama.
6. Serengeti National Park inapatika kati
ya futi 3020 na futi 6,070 juu ya usawa wa
bahari. Hali ya hewa yake kwa ujumla ni
kavu lakini inapata mvua nyingi katika
miezi ya Juni na Julai
7. Serengeti kwa kiasi kikubwa ni ya
uoto wa savannah na vichaka
vilivyotawanyika na ambavyo ni bora kwa
ajili ya wanyama walao nyasi na nzuri
kwa ajili ya wanyama walao nyama pia.
Miongoni mwa wanyama wapatikanao
hapa ni pamoja na, pundamilia, tembo,
twiga, nyumbu, swala , paa na nyati.
Miongoni mwa wanyama walao nyama
wanaopatikana ni pamoja na simba, duma
, chui, fisi , mbweha, nk
8. Serengeti ni chimbuko la jamii
maarufu ya Wamasai kabla ya
kuhamishiwa katika maeneo ya mamlaka
ya hifadhi ya Ngorongoro mnamo mwaka
1959 . Wamasai ni moja ya jumuiya za
Kiafrika kwamba ambazo bado huishi kwa
kuzingatia mila zao za kale na utamaduni
kama vile tohara , ngoma na kafara.
9. Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro awali
lilikuwa sehemu ya hifadhi ya serengeti
mpaka 1951 wakati Uingereza
walipolitenga kwa ajili ya utafiti kama
binadamu na wanyamapori wanaweza
kuishi pamoja katika sehemu moja bila ya
kuathirana.
10. Kwa mara ya kwanza utafiti wa
kina juu ya mazingira ya Serengeti
ulifanywa na raia wawili wa Ujerumani
( baba na mwana ) , Dk Bernhard na
Michael Grizmek . Maelezo ya matokeo ya
tafiti za Serengeti ziliwekwa na
kuhifadhiwa kama kumbukumbu katika
kitabu chao maarufu kinachoitwa
“Serengeti shall never die.”
Katepahot tutakujuza na kukufahamisha juu
ya utajiri wa nchi yetu, kwani tunaamini
Tanzania ni nchi ya Maajabu ya kuvutia.
#UTALII KWA WOTE#
Mfumi wa uhamaji wa Nyumbu wa Serengeti
Misururu ya nyumbu wakihama kutoka upande
mmoja kwenda mwingine katika hifadhi ya
Serengeti
Binadamu wa kale aliepata kuishi maeneo ya
serengeti miaka milion 2 iliyopita
Pundamila pia huama pamoja na nyumbu
katika hifadhi ya Serengeti
Nyumbu wakivuka moja ya mito
inayopatikana Serengeti
Kipindi cha mvua Serengeti
Wamasai wakiwinda na silaha za jadi
Dr. Bernard Grizmek na mwanae Michael
Grizmek wakiwa katika tafiti zao kwenye
Hifadhi ya Serengeti picha zote hizi hapa chini kuhusu habari hii
0 Comments