BREAKING NEWS: Ajali iliyohusisha Basi la Super Shem na Hiace yaua watu zaidi ya 10 Mwanza

Basi la Super Shem lililokuwa likitokea Mbeya Kuelekea Mwanza limepata ajali katika eneo la Hungamalwa wilayani Kwimba mkoani Mwanza.
Taarifa zinasema basi hilo limepata ajali mida ya saa kumi na Moja baada ya kuvaana na Hiace, moja wa mashuhuda wa ajali hiyo amesema basi hilo lilikuwa katika mwendo kasi hali iliyomfanya dereva kushindwa kulimudu na kugongana na hiace hiyo.
Mpaka sasa watu walioripotiwa kufa ni 11, na idadi ya majeruhi bado haijajulikana ila wote wamepelekwa hospitali kwa matibabu, WWW.KATEPAHOT.BLOGSPOT.COM tutaendelea kukupa Taarifa zaidi.

Post a Comment

0 Comments