WATU wanne wamenusurika kuuwawa ziwa Victoria


WATU wanne wamenusurika kuuwawa na wananchi wenye hasira wakiwatuhumu kufanya uvuvi haramu wa kutumia sumu ndani ya ziwa Victoria.
Tukio la kukamtwa watu hao limetokea jana majira ya saa kumi na mbili alfajiri katika mwalo wa Kichuguuni kijiji cha Lukumbo kata ya Butundwe wilaya na Mkoa wa Geita, ambapo kwa mujibu wa mashuhuda, watuhumiwa hao walikamatwa na samaki wanaodhaniwa kuvuliwa kwa sumu.
Baada ya kuhojiwa, watuhumiwa hao walikiri kufanya uvuvi haramu ndani ya ziwa hilo, na kuwataja tu waliowatuma kutoka jijini Mwanza ambao hata hivyo majina yao yamehifadhiwa kwa sababu za uchunguzi, na kwa mujibu wa Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ambaye ni mkuu wa wilaya ya Geita HERMAN KAPUFI watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani.
Hivi karibuni mkuu huyo wa wilaya ya Geita alifanya ziara kwenye visiwa vinavyozunguka ziwa Victoria na kutoa elimu juu ya madhara ya uvuvi haramu ambapo alimtaka kila mwananchi kuwa mlinzi wa mwenzake.

Post a Comment

0 Comments