Jibu la ney kuhusu t.touch

Baada ya Producer Mr.Touch kujitoa kwenye studio za Free Nation zinazomilikiwa na rapa Nay wa Mitego,rapa huyo amesema hana tatizo na Mr.T Touch licha ya producer huyo kudai kuwa Ney alikuwa akimnyonya.
Akiongea kwenye kipindi cha Funiko Base cha radio 5 Nay amesema anamchukulia Mr.T Touch kama mtoto aliyefikia umri fulani na kujiona amekua na yeye kama mzazi hana budi kumwacha afanye vile ambavyo yeye anaona ni sahihi kwani amekuwa kama mlezi wake kwa muda mrefu sasa.
Ni kweli,mimi na Mr.T hatuko pamoja,lakini mimi sina tatizo na Mr.T,namchukulia kama mdogo wangu,nimekuwa naye muda mrefu.Unajua inafika time kila mtu anaamua kufanya kitu ambacho anahisi ni sahihi kwake,me simlaumu.Mimi ni kama mlezi kwake nikisema nina ugomvi nae ntakuwa sio mlezi mzuri” alisema Nay wa Mitego.

Post a Comment

0 Comments