Pop staa Justin Bieber ambaye kwa sasa anatajwa kuwa miongoni mwa wasanii wa pop maarufu kwa utundo na skendo za mapenzi amepiga chini mchongo wa kuigiza kama shoga kwenye filamu ya ‘Uber Girl’ .
Justin alisema hataweza kufanya filamu hio mpaka waondoe sehemu iliyomtaka ambusu dansa wake wa kiume na kushikwa makalio na dansa huyo.
Mwandishi mwenza wa filamu hiyo Pete O’Neill ameuambia mtandao wa Page Six kuwa ukiachana na Justin, watu wengine maarufu kwenye filamu hio ni pamoja na Selena Gomez na Ariana Grande.


0 Comments