PICHA 5: Gari jipya ya Cristiano Ronaldo aliyoinunua Tsh bilioni 4.9

Baada ya michuano ya Euro 2016kumalizika na timu ya taifa ya Urenoinayoongozwa na nahodha wakeCristiano Ronaldo kutwaa taji hilo, headlines zimekuwa nyingi baada ya staa huyo kushinda Kombe hilo kwa mara ya kwanza katika historia ya maisha yake

Ronaldo baada ya kutwaa Euro 2016aliripotiwa kutoa msaada bonansi yake yote aliyopewa, ila headlines za staa huyo hazijaishia hapo, kwani ameamua kununua gari jipya ikiwa siku chache zimepita toka afanikiwe kutwaa Kombe la Euro 2016, kitendo ambacho kinatafsirika kama kuamua kujizawadia zawadi hiyo.

Staa huyo wa Real Madrid amenunua gari aina ya Bugatti Veyron 16.4 Grand Sport, gari ambalo lina thamani ya pound milioni 1.7 kiasi ambacho ni zaidi ya bilioni 4.9 za kitanzania, gari aina ya Bugatti Veyron 16.4 Grand Sportaliyoinunua Ronaldo zinatajwa kuwa hadi sasa zimetengenezwa 450 tu, hiyo inatokana na thamani ya gari yenyewe.


Post a Comment

0 Comments