Rapa Desiigner hivi karibuni amefunguka kuwa alipigwa risasi ya paja akiwa na umri wa miaka 14. Desiigner ni msanii aliyeng’ara na wimbo wa “Panda,” na kupewa dili la lebel na rapa Kanye Wests kwenye lebel yake ya ‘ G.O.O.D. na anatoka mjini Brooklyn, New York.
Akiongea na This Is 50 Desiigner anasema “ Sikuwa mtoto mzuri, nilikuwa mitaani nikifanya mamo ya kijinga, Nikiwa na miaka 14 nilipigwa risasi na kuka hospitalini kwa zaidi ya dakika 10 au 30, hapo ndipo nilipoamua kufata mambo yangu, na baada ya hapo nilibadilisha maisha yangu na kuanza kwenda studio badala ya mitaani “.
Desiigner anasema alirekodi wimbo wake wa kwanza ulioitwa “ Jackie Chan,” akiwa ma miaka 14.




0 Comments