Mwigizaji mkubwa wa show ya Empire Terrence Howard aliponea chupuchupu kufukuzwa kazi na viongozi wa show hio kutokana na makosa tofauti yaliyomkabili mwaka jana.
Viongozi wa show ya Empire walichoshwa na tuhuma tofauti zilizomkabili star huyu kama Udhalilishaji wa majumbani dhidi ya aliyekuwa mke wake kosa ambalo lilimfikisha Terrence Howard mahakamani.
Taarifa hizi zimefichuka baada ya bwana Terrence Howard ’47’ kuchelewesha malipo ya kampuni inayosimamia vipaji ya Authentic Talent inayosimami kazi za Terrence anayeigiza kama Lucious Lyon kwenye Empire.
Kampuni hii imedai haijalipwa pesa za dili mbili kubwa za Terrence ambazo ni kuigiza Empire msimu wa pili na watatu, kampuni hii ndio ilihusika kwenye kusuluhisha matatizo kati yake na viongozi wa Empire.



0 Comments